To advertise here, call: +255 655 611699

About Us

Shirika la FUNGUKA TANZANIA ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo, mtazamo na nia ya kuisaidia jamii kuongeza ushiriki wa vijana, wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi katika shughuli za ujasiriamali (kilimo, biashara na ufugaji) ili kuongeza uzalishaji, kuongeza kipato, kupanua biashara na kupunguza tatizo la ajira na umasikini. 


DIRA YETU


Kuondoa tatizo la ajira kwa vijana, kufuta umaskini na kuwa na matumizi yenye tija ya rasilimali na fursa zilizopo hapa nchini.

LENGO KUU

Kuiwezesha jamii kukuza uchumi na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana kwa kuongeza uzalishaji na uwekezaji kwenye sekta ya biashara, viwanda, soko la hisa, huduma, kilimo, na ufugaji.