To advertise here, call: +255 655 611699

Nufaika na zao la muhogo


Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Pia makabila mengine husaga unga wa mihogo iliyokaushwa(makopa/udaga) na kuchanganya na mahindi au nafaka nyingine kisha kuutumia kwa chakula. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani
Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.
MAMBO YA KUZINGATIA
i.              Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimethibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
    • Naliendele: huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanznia miezi tisa toka ipandwe.
    • Kiroba: Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
    ii.        Mbinu bora za kilimo cha muhogo
Uandaaji wa shamba:
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
  Kufyeka shamba
Kung'oa na kuchoma visiki
  Kulima na kutengeneza matuta
   iii.        Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda:
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.
   iv.        Upanadaji: Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
  Kulaza ardhini
  Kusimamisha wima
  kuinamisha
    v.        Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

   vi.        Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.


 vii.        Palizi:
a.    Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
b.    Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
c.    Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
d.    Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.
viii.        Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

Share on Google Plus

About Funguka Tanzania

0 comments:

Post a Comment