To advertise here, call: +255 655 611699

JINSI YA KUANDAA MVINYO WA NDIZI (BANANA WINE)

          
Ndizi ni tunda lililozoeleka kutumika na watu wengi duniani, tunda hilo linaweza pia kutumika kuandaa mvinyo ambao unaweza kutumika kwa familia na pia unaweza kuuzwa na kujipatia kipato. Leo tumewaletea hatua kwa hatua namna ya kuandaa mvinyo wa ndizi (banana wine) kama ifuatavyo:
     
                               HATUA  YA  KWANZA :

*  Chukua   ndizi  kg.3  zilizo  menywa  maganda  na  ambazo  zimeiva  vizuri, katakata   vipande  vidogo  na  weka  katika  chombo  ambacho  utatumia  kuchachulia  wine  yako.


*  Baada  ya  kupata  hivyo  vipande  vidogo  vidogo , vichanganye  kwenye  maji  lita  ( 5 )  na   baada  ya  hapo  chemsha   kwa  muda  wa  dakika  30.

* Acha  mchanganyiko  wako  huo  upoe.

                                                    HATUA   YA  PILI

*  Changanya  mchanganyiko  wa  ndizi  na  sukari  kikombe  kimoja   cha  chai, koroga  kisha  changanya  na  amira   vijiko  vinne (  4  )  vya  sukari, koroga  tena.

*  Acha  kwa  muda  wa  siku  nne,   siku  ya  nne  utakapo  kwenda  kuitazama  wine  yako  utakuta  povu, hii  ina  maana  kuwa  wine  yako  itakuwa  imeanza  kuchachuka   vizuri.

*  Siku  ya  tano  (  5  )  chuja  wine  yako  vizuri  kwa  kutumia  kitambaa  lakini  bila  kufinyanga, iache  wine  imwagike  yenyewe.

                                               HATUA  YA  TATU 

* Iweke   wine  yako  kwenye  chombo  cha  kutolea  hewa  na   kupunguza  gas  kwa  siku  1  mpaka  miezi  3.

*  Baada  ya  siku  21  wine  yako  itakuwa  tayari.
Share on Google Plus

About Funguka Tanzania

0 comments:

Post a Comment