To advertise here, call: +255 655 611699

Jinsi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara.


Moja kati ya changamoto tulizonazo vijana tunapofikiri kufanya biashara au kuanzisha mradi wowote ni jinsi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara hiyo. Katika kipengele hiki naenda kujadili changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha. Leo tutajadili changamoto ya ukosekanaji wa mitaji na jinsi ya kuipata. Kabla hatujaanza kujadili changamoto hii naomba niweke maoni ya baadhi ya watu niliojadili nao kuhusu suala hili
kwa wasomi wote wenye taaluma ambao hawana ajira wala kazi niliowauliza kwanini hawajaanzisha biashara au kujiajiri wengi wao majibu yao yalikuwa:
1.     kila nikifikiria kuanza kuijajiri nashindwa kutokana na kipato cha kuanzia biashara.. je nifanyeje niweze kupata kipato cha kujiajiri?
2.    Napenda sana kufanya biashara ila tatizo ni eneo la kufanyia, ama kodi nikubwa sana na maeneo hakuna.
3.    changamoto ni kutokuwa na mitaji ya kukusaidia kuanzisha biashara, hata kama ukipata fursa, swala linabakia mitaji nimtaji, kwani ubunifu unaendana na fedha ya kuanzia.
4.    Namna ya kupata mtaji. Biashara niiwazayo ni Duka la vifaa vya ujenzi na Umeme, duka la vipodozi, duka la spea za magari na pikipiki, duka la kuuza nguo, n.k. Kodi ya eneo husika ni kama efu sitini mpaka laki moja kwa mwezi!!
5.    Ukosefu wa mtaji na sijui nitumie njia gani kupata.
Hayo hapo juu ni baadhi ya maoni ya wasomi waliopo mtaani kwa kukosa ajira kuhusiana na changamoto ya mtaji.

Kikwazo kikubwa cha kuanza au kukuza biashara sio mtaji.

Ndio nasema kwamba tatizo linalokuzuia wewe kuanza au kukuza biashara sio mtaji bali ni utayari wa mtu wewe mwenyewe. Mtaji umekuwa ukitumika kama sababu ya watu kutokuumiza vichwa ili kujua wanawezaje kuingia kwenye biashara. Kila mtu utakayeongea nae kuhusu biashara ataanza na tatizo ni mtaji. Ukimuuliza ni mtaji kiasi gani anahitaji atakutajia, ukimuuliza ukipata kiasi hicho utakitumiaji hawezi kukupa mchanganuo wenye mantiki maana hajawahi kufikia hatua ya kuchanganua hiyo biashara. Ukimuuliza kama hutapata kiasi chote hicho unachotaka unaweza kuanzia kiasi gani halafu ukaendelea kukua pia anakosa majibu. Hii ndio inanisababisha niamini kwamba kikwazo cha kwanza sio mtaji bali ni utayari wa mtu mwenyewe.

Wakati nafikiria njia za kupata mtaji wa kuanzia biashara miaka mitatu iliyopita, niliamua kuchukua kazi ambayo haikuwa na malipo makubwa. Wafanyakazi niliowakuta pale kila tulipokuwa tunazungumzia biashara walikuwa wakilalamikia mtaji. Nilifanya kazi pale kwa mwaka mmoja, nikapata mtaji wa kuanzia biashara, lakini mpaka leo nikikutana na wafanyakazi wale wanasema tatizo ni mtaji. Sasa hebu niambie kama unasema tatizo ni mtaji kwa zaidi ya miaka miwili bado unaendelea kuamini tatizo ni mtaji kweli? Hapana, tatizo ni wewe mwenyewe.
Kuna njia nyingi sana za kutatua tatizo lako hilo la kushindwa kupata mtaji. Hapa nitazungumzia tano unazoweza kuanza kufanya leo na siku zijazo ukasahau kabisa kuhusu tatizo hilo.
1. Tumia akiba zako, au anza kuweka akiba.
Kama kuna akiba zozote ambazo umekuwa unajiwekea kwa muda unaweza kuzitumia kwa kuanzia biashara. Kama huna akiba yoyote anza sasa kujiwekea akiba na jipe muda unaohitaji ili kufikisha kiwango cha mtaji unachotaka.
2. Chukua kazi hata yenye maslahi kidogo.
Kama ndio umemaliza shule na hujapata ajira na pia huna mshahara wa kuanzia nakushauri uchukue kazi yoyote unayoweza kupata hata kama ina maslahi kidogo. Lengo lako litakuwa ni kukusanya mtaji na hivyo utaifanya kazi hiyo kwa kipindi fulani na kisha kuachana nayo. Inabidi ukubali kuteseka kwa muda kidogo ili uweze kufika kule unakotazamia. Sasa kama utaniambia kwamba wewe ni msomi na kuna kazi huwezi kufanya, nitakuambia uendelee kuimba tatizo ni mtaji.
3. Anza kidogo.
Unapoanza biashara hasa pale unapoanzia sifuri ni vigumu sana kuweza kupata kiasi chote cha fedha unachohitaji. Unaweza kuanza kidogo na baadae ukaendelea kukua na pia kujifunza. Jua ni kiasi gani unahitaji kama mtaji na gawa kwenye kiasi kidogo ambacho unaweza kuanzia. Ukisema usubiri mpaka upate kiasi kikubwa unachofikiria itakuchukua muda mrefu sana na baadae utakata tamaa.
4. Ungana na mwenzako mwenye mawazo kama yako.
Unaweza kuungana na mwenzako au wenzako wenye mawazo kama yako na mkaunganisha fedha kidogo mlizo nazo na kuweza kuanza biashara. Hii ni njia nzuri sana ya kuweza kuunganisha mitaji kidogo ambayo unaweza kuitumia na ukafikia mafanikio makubwa.
5.  Uza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa navyo.
Hapa nakwenda moja kwa moja kwa vijana hasa waliomaliza masomo karibuni. Kama unataka kuanza biashara ila huna mtaji, nakushauri uuze vitu vingi ambavyo ulinunua ukiwa masomoni ambavyo kwa sasa hauna uhitaji mkubwa navyo. Anza kwa kuuza TV, sub-woofer, Friji, nusu ya nguo ulizonazo sasa, kwa sababu hutazivaa, uza smartphone uliyonayo sasa, ni ya gharama kubwa(wengine wanatumia simu ya million na zaidi) na kama mpaka sasa huna biashara haina msaada wowote kwako zaidi ya kukulazimu kukopa salio ili uweke bando kujua wenzio wameweka nini mtandaoni, uza ili kupata mtaji, biashara yako itakurudishia na zaidi. Ukipiga mahesabu ya haraka haraka unaweza kupata kiasi fulani cha fedha kinachotosha kuanzia kama utauza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa kwa sasa.
Kama nilivyosema hapo juu, tatizo kubwa sio mtaji bali mipango yako mwenyewe na kiasi gani unahitaji kuingia kwneye biashara. Kama kweli unataka kuingia kwenye biashara, jipe mwaka mmoja tu wa kukusanya mtaji, katika mwaka huo, fanya kila kitakachopita mbele ya macho yako, ila kiwe halali kuweza kupata mtaji unaohitaji. Kuendelea kulalamika kwamba kinachokuzuia ni mtaji hakutakusaidia chochote zaidi ya kuendelea kuwa na maisha magumu.
Funguka, anza sasa, asilimia tisini ya mtaji unaohitaji ni akili yako, anza kuitumia.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kupata mtaji wa kuanza biashara.



Share on Google Plus

About Funguka Tanzania

8 comments:

  1. Ahsante sana kwa mawazo chanya

    ReplyDelete
  2. Safi Sana but baadhi ya vijana wanawaza kuanza na mtaji mkubwa ambao hawawez kupata

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Naomba kuuliza mkuu Mimi nina hardware na mbao pia ninazo Ila biashara bado nichanga je naitangaza vipo biashara yanga ili iweze kujulikana kwa halaka zaidi

    ReplyDelete