Upandaji miti ikiwemo Miti ya Matunda ni moja kati
ya njia inayoweza kuwakwamua vijana kutokana na tatizo la ajira na umasikini. Ipo
miembe iliyoboreshwa, miembe hiyo imetokana na kuunganishwa kwa miembe miwili tofauti. teknolojia
ya ubebeshaji wa mimea inapelekea upatikanaji wa miembe yenye sifa ambazo
wakulima wanazihitaji mfano ladha nzuri, ukubwa wa matunda na matunda yasiyo na
nyuzinyuzi.
Miembe ya kubebeshwa huchukua muda
mfupi kutoa mavuno kwani mwembe unaweza kutoa matunda ndani ya miaka miwili na
nusu hadi mitatu tofauti na miembe ya asili ambayo huchukua muda si chini ya
miaka mitano tangu kupandwa kuanza kutoa matunda. Na kwamba, embe la mwembe
uliobebeshwa lililokomaa huwa linauwezo wa kuwa na kilo moja hadi kilo moja na
nusu.
0 comments:
Post a Comment