Mwanamke akipenda anapenda kweli!
Mwanamke akikupenda anakuwa na furaha, anakuwa anajivunia kuwa na wewe,
na hujihisi furaha kuongea na wewe.
Hupenda awe rafiki wa rafiki zako na ndugu zako, uvipendavyo na yeye
atavipenda, atabadilisha mtindo wake wa maisha kuendana na mtindo wako.
Haitajalisha ni kiasi gani utamuudhi, atakusamehe hata kabla hujamuomba
msamaha, atachokifanya ni kusubiri tu umuombe msamaha kuthibitisha kama
kweli umejutia kosa lako.
Atajaribu kuwa na wivu na atakulinda kwani atahitaji uwe wake, wake peke
yake na sio ku share.
Atawakataa wengine wote wanaomtongoza kwa sababu
ameona kesho yake ipo mikononi mwako.
Haitajalisha ni kiasi gani uko mbali na yeye, atajilinda kwa ajili yako.
Atalike na ku comment kila kitu unachoweka facebook hata kama ni cha
kipuuzi (hahaahaa).
Atakujibu kwa wakati text zako either watsapp, za kawaida au inbox ya
fb. Hatajali kama unampa pesa au laa, kama ni tajiri au laa kwa sababu
lengo lake ni kujenga maisha na wewe na sio kupass time ameona
potentials kwako.
Atakuonyesha marafiki zake na ndugu zake, kwa sababu anajivunia kuwa
mpenzi wako.
Tafadhali sana, muangalie mwanamke huyo, moyo wake umejawa na mapenzi,
anastahili kutunzwa na kupendwa kama almasi.
Lakini tatizo kubwa la hawa "wavulana" (baadhi yao) baada ya kumfanya
akupende zaidi, baada ya kupoteza muda wake juu yako, baada ya kuwakataa
wanaume wengine ambapo kimsingi wengine walikuwa tayari kumuoa, baada
ya kumuacha akutambulishe kwa ndugu zake na marafiki sasa unamuacha,
unamkataa kwa mbwembwe nyingi, unamuacha akiwa na maumivu na aibu kubwa
kwamba atawaambia nini wazazi wake, ndugu na marafiki, atatambulisha
wangapi?
Na akiulizwa yuko wapi yule uliyetutambulisha? Awajibu nini!? Ofcoz
atakachofanya ni kuinamisha kichwa huku ameshika mashavu! Hana jibu ni
aibu na maumivu makubwa kwa kuwa alikupenda kwa dhati.
Mbona mnawaweka katika wakati mgumu wanawake waliopewa moyo wa kupenda?
Brothers, usimfanye mwanamke wako ajute kwanini alipenda, usifanye
wengine wamcheke na kumdhihaki. Timiza ahadi yako, kama amekukosea na
kukuomba msamaha jaribu kumpa nafasi ya pili. Kila mtu anahitaji nafasi
ya pili ili aweze kurekebisha pale alipokosea.
Na nyie vijamaa mnaokua sasa, miaka 14 na kuendelea msiige tabia ya sisi
kaka zenu, hiyo sio tabia njema kabisa. Jifunzeni kuheshimu hisia za
mtu. Kujeruhiwa kihisia kunauma kuliko maumivu ya risasi.
Kama huna future nae usimtongoze na kumpa mimba.
0 comments:
Post a Comment