To advertise here, call: +255 655 611699

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUANDAA CHAKULA CHA KUKU

Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa. Chakula hicho lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko wa vyakula vifuatavyo:
         i.            Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, samaki, dagaa, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti.
        ii.            Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, michicha, majani ya mpapai na nyasi mbichi.
      iii.            Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa, mifupa iliyosagwa na chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama Kalsiamu na Fosforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole, kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho.
Maji ni muhimu sana kwani husaidia kulainisha na kurahisisha usagaji wa chakula, na kupunguzajoto. Wakati wajoto kali kuku wapewe maji mengi.
Kabla ya Kutengeneza Chakula Lazima Mtengenezaji Ajue haya Yafuatayo:-
         i.            Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbali mbali.
        ii.            Kiasi cha viinilishe vinavyohitajika kwa kuzingatia umri na aina tofauti ya kuku; kwa mfano vifaranga wanahitaji protini asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokua asilimia 17 hadi 19 na kuku wa mayai asimilia 15 hadi 17. Vile vile madini aina ya Kalsiamu kiasi cha asilimia tatu hadi nne kinahitajika kwa kuku wa mayai na asilimia moja kwa kuku wa nyama na vifaranga.
      iii.            Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbali mbali: Ili mtengenezaji aweze kutengeneza chakula bora ni muhimu afuate kiwango cha uchanganyaji kilichopendekezwa Kiasi cha aina moja ya chakula kinapozidi kinaweza kuleta madhara.
Jedwali lifuatalo linaonyesha kiwango kinachotakiwa kwa baadhi ya vyakula.
Vyakula na Viwango Vinavyohitajika katika Asilimia 100
Aina ya Chakula
Kiwango cha Uchanganyaji (%)
Vyakula
Vifaranga
Kuku wa Nyama
Kuku wa Mayai
Mahindi
70
70
70
Ulezi
20
40
40
Mtama
20
30
30
Mpunga
40
70
70
Ngano
5
40
40
Pumba za mahindi
10
20
20
Pumba za Mpunga
10
20
20
Pumba za Mtama
10
20
20
Pumba za Ngano
5
15
15
Mashudu ya nazi
10
30
40
Mashudu ya Pamba
5
10
5
Mashudu ya Alizeti
10
20
20
Mashudu ya Ufuta
10
10
5
Damu iliyokaushvva
5
5
5
Mifupa iliyosagwa
5
5
7.5
Dagaa
10
5
5
Lusina iliyosagwa
(Lucerne meal) Lukina
5
5
5
(Lcuecana meal)
2.5
5
5
Chokaa
5
5
5
Chumvi
0.5
0.5
0.5
Soya
10
20
20
 Kuhusu kiasi cha viinilishe kama protini, wanga, madini na vitamini vilivyomo kwenye aina za vyakula vitakavyochanganywa, Mfugaji anashauriwa amuone mtaalamu wa mifugo aliyekaribu naye aweze kumsaidia na kumpa ushauri zaidi.·
 Mchanganyiko uwe na zaidi ya aina moja ya vyakula kwa mfano vyakula vya kujenga mwili vitokanavyo na wanyama na mimea.·
Mifano ya kutengeneza kilo 100 za chakula cha kuku:-
 Mfano wa chakula cha vifaranga kuanzia siku ya kwanza hadi majuma manne.·
Vyakula
Kiasi (Kg)
Mahindi
30.00
Pumba za Mahindi
20.00
Soya
18.00
Mashudu ya Alizeti
20.50
Dagaa
5.00
Mifupa iliyosagwa
4.00
Chumvi
0.50
Vitamini
2.00
 Jumla
100.00
 Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia Juma la nne hadi la nane.·
Vyakula
Kiasi (kg)
Mahindi
45.00
Pumba za Mahindi
20.00
Mashudu ya pamba
5.00
Soya
20.00
Dagaa
2.50
Mifupa iliyosagwa
5.00
Chumvi
0.50
Vitamini
2.00
 Jumla
100.00
 Mfano wa chahula cha kuku wa mayai kuanzia Juma la nane hndi la ishirini.·
(a)
(b)
Vyakula
Kiasi (Kg)
Vyakula
Kiasi (Kg)
Mahindi
45.00
Mahindi
45.00
Pumba za mahindi
25.00
Pumba za mahindi
30.00
Soya
5.00
Soya
5.00
MashuduyaAlizeti
10.00
Mashudu ya pamba
5.00
Dagaa
4.00
Dagaa iliyokaushwa
4.00
Damu
3.00
Mifupa iliyosagwa
2.50
Chokaa
3.00
Chokaa
3.00
Chumvi
0.50
Chumvi
0.50
Vitamini
2.00
Vitamini
2.00
 Jumla
100.00
100.00
 Mfano chakula cha kuku wa Mayai kuanzia Juma la lshirini na kuendelea:·
(a)
(b)
Vvakula
Kiasi (Kg)
Vvakula
Kiasi (kg)
Mahindi
50.00
Mahindi
40.00
Pumba za mahindi
15.00
Pumba za mahindi
25.00
Mashudu ya Pamba
5.00
Mtama
5.00
Soya
18.00
Mashudu ya Alizeti
10.00
Dagaa
4.50
Dagaa
4.00
Mifupa iliyosagwa
3.00
Damu ilyosagwa
5.00
Chokaa
2.00
Mifupa iliyosagwa
4.50
Chumvi
0.50
Chokaa
4.00
Vitamini
2.00
Chumvi
0.50
 Jumla
100.00
Vitamini
2.00
 Jumla
100.00


Share on Google Plus

About Funguka Tanzania

0 comments:

Post a Comment