Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya
kusaidia watu maskini zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa
kufuga kuku
Bilionea huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa
muhimu katika kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo
tayari umewavutia na kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la
Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Bwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata
zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka. Mtu hutajwa kuwa maskini iwapo anapata Dola 700
pekee kwa mwaka.
Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia zaidi ya asilimia 30 ya watu
wanaoshi mashambani Kusini mwa Jangwa la Sahara ili wapate huduma ya kufuga
kuku wa hali ya juu mbao watachanjwa. Alisema hatua hiyo itaongeza watu
wanaofuga kuku kwa asilimia tano.
Ananukuliwa akisema kuwa kuku huongezeka maradufu na kwa hivyo hakuna
uekezaji ulio na mapato mazuri kwa asilimia ya juu kuliko ufugaji kuku.
Alisema hayo alipokuwa akianzisha mradi huo jijini New York.
Anashirikiana na shirika na kutoa misaada kwa maskini la Heifer International.
Watu milioni 800 huishi katika hali ya umaskini hohehahe, kulingana na
takwimu za Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment